DISQUS SHORTNAME

Beyonce, Solange na Jay Z watoatamko la pamoja kuhusu tukio laSolange kumpiga Jigga ndani yalifti

Beyonce, mume wake Jay Z pamoja na dada yake  Solange Knowles wamevunja ukimya kwa kutoa  tamko la pamoja kuelezea tukio la ugomvi wa kif...


Beyonce, mume wake Jay Z pamoja na dada yake  Solange Knowles wamevunja ukimya kwa kutoa  tamko la pamoja kuelezea tukio la ugomvi wa kifamilia lililotokea May 5 ndani ya lift na video yake kuvuja.
“Kama matokeo ya kuvuja kwa video ya ‘elevator security’ kutokea Jumatatu, Mei 5, kumekuwa na vumi mwingi kuhusu chanzo cha tukio hilo la bahati mbaya” Walieleza katika tamko hilo kwa  shirika la habari The Associated Press. Waliendelea, “lakini kitu cha muhimu ni kwamba familia yetu  imelifanyia kazi swala hilo..Jay na Solange kila mmoja amewajibika kwa sehemu yake kwa kile  kilichotokea. Wote wawili wameombana radhi kila mmoja na tumeendelea kuwa familia moja. Taarifa za Solange kulewa au kuonesha tabia isiyoeleweka jioni ile ni za uongo.”  Pamoja na kutozungumzia sababu za kilichotokea  lakini walitisha kuwa wameyamaliza, “Mwisho wa siku kila familia huwa na matatizo na sisi hatuna tofauti na familia zingine.
Tunapendana na kubwa kuliko yote sisi ni familia. Tumeyaacha haya yamepita na matumaini yetu kila mtu mwingine yoyote atafanya hivyo pia.” Video isiyokuwa na sauti iliyovuja Jumatatu na  kuwekwa TMZ ilimuonesha dada yake Beyonce, Solange akimshambulia shemeji yake Jay Z ndani ya lift, na baadae kuwa tukio lililozungumziwa kila pande ya dunia kama habari kubwa.

Related

KWINGINEKO DUNIANI 6615936182153454561

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item