DISQUS SHORTNAME

ADAM KUAMBIANA KUZIKWA ALIPOZIKWA KANUMBA

SHABIKI wa Yanga na msanii wa filamu za maigizo nchini kutoka kambi ya Bongo Muvi , aliyejizolea umaarufu miaka ya hivi karibuni , Adam K...

SHABIKI wa Yanga na msanii wa filamu za
maigizo nchini kutoka kambi ya Bongo Muvi ,
aliyejizolea umaarufu miaka ya hivi karibuni ,
Adam Kuambiana aliyeaga dunia juzi
Jumamosi , anatarajiwa kuzikwa kesho
Jumanne kwenye makaburi ya Kinondoni jijini
Dar es Salaam alipozikwa msanii mwenzake ,Steven Kanumba .

Akizungumza na Championi Jumatatu , jana,
Rais wa Bongo Muvi, Steve Mengere ‘ Steve
Nyerere’ , alisema ratiba iliyopo ni kesho
asubuhi waombolezaji kudamkia Muhimbili
kuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka
Viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya
mazishi ambayo yatafanyika katika makaburi
ya Kinondoni jijini .
Kiongozi huyo wa Bongo Muvi alisema bado
hawajampata kiongozi wa kuongoza mazishi
hayo lakini mpaka tunaelekea mitamboni
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete
alithibitisha kuhudhuria mazishi hayo .
Akizungumza na gazeti hili rafiki wa
marehemu ambaye ni msanii mwenzake na
shabiki mwenzake wa Wanajangwani , Yanga,
Rashid Makupa ‘ Kupa ’ , alisema anakumbuka
mechi ya mwisho kwenda naye uwanjani
kuiangalia ni ile ya Simba na Yanga
iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam ambapo matokeo yalikuwa sare ya
bao 1-1 .
Kupa alisema katika vitu ambavyo
anakumbuka kwa marehemu , ni kwamba
alikuwa hapendi kitendo cha Yanga kukosa
ushindi.

Related

BONGO MOVIE 2114120454226505838

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item