ULEVI NI NOMA BINTI WA KIGOGO AFANYIWA MBAYA
ULEVI noma! Ndivyo unavyoweza kusema kuhusu kilichomtokea mtoto wa kigogo mmoja aishie Masaki ambaye alijikuta akifanyiwa kitu mbaya...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/12/ulevi-ni-noma-binti-wa-kigogo-afanyiwa.html
ULEVI noma! Ndivyo unavyoweza kusema kuhusu
kilichomtokea mtoto wa kigogo mmoja aishie Masaki ambaye alijikuta
akifanyiwa kitu mbaya ndani ya maji kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi,
eneo la Coco jijini Dar, Jumamosi iliyopita.
Chanzo kilichoshuhudia tukio hilo kilishadadia maneno kwa mpigapicha wetu kwa kusema kuwa, wakati mrembo huyo anaenda kuogelea ndipo alipoangukia kwenye mikono ya njemba mmoja aliyekuwa akifanya mazoezi pembeni mwa ufukwe huo ambapo pia alikutana na wachezaji wa Azam FC waliokuwa wakifanya mazoezi mambo yakaharibika.
“Wakati anawafuata wale wachezaji, redio za watu wa bajaj zilikuwa zimefungulia muziki kwa sauti, akawa anacheza, jamaa walipoona vile wakaongeza sauti na kumwekea wimbo wa Davido wa Aye, dah, ndio akachizika kabisa, jinsi alivyokuwa akikata mauno na nguo alizovaa, aliwachanganya kabisa wachezaji wa Azam ambao walikuwa wakimtumbulia macho kwa udenda,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuwapagawisha wachezaji hao, binti huyo alipomfuata njemba mmoja aliyekuwa kando na kumuomba amfundishe kuogelea, jamaa akachukua tairi la gari na kumwingiza baharini ambako alianza makeke ya kumfundisha huku wakizamia kuonesha kuna kamchezo kachafu kanaendelea.
Baadaye akiwa kama aliyeshtuka, alikurupuka majini humo na kutoka nje akikimbia, akimuacha njemba aliyekuwa naye baharini akimtumbulia macho ya kutoamini kilichotokea.
