DISQUS SHORTNAME

MAMA KANUMBA AMWAGA ‘SUMU’ ZA MWANAYE

MAMA  wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema kama kuna msanii anataka kufikia ‘levo’ za mwanaye b...

MAMA wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema kama kuna msanii anataka kufikia ‘levo’ za mwanaye basi asali sana.

Mama wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.

Akifunguka mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, mama Kanumba alisema pengo la mwanaye katika sanaa linaonekana wazi hivyo ni vyema kwa anayetaka kuliziba kufuata nyayo zake.

”Miongoni mwa siri kubwa za mafanikio kwa mwanangu zilizomfanya awike kuliko wengine ni kupenda kuthubutu, kusali sana na kutokuwa na wivu wa maendeleo kwa kujiepusha na majungu.

Marehemu Steven Kanumba,enzi za uhai wake.

“Tatizo wasanii wetu hawa hawapendi kuthubutu wamekalia tu kufanyiana majungu, hawapendi kuona mwenzao anafanikiwa wanaanza kumfitini, ni vizuri wangejifunza kitu kwa Kanumba ambaye alipenda kuthubutu,” alisema mama Kanumba.

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item