AMFUMANIA MUMEWE, ASAULA!
HATARI! Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Tatu Ikoko mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, hivi karibuni alifunga mtaa kwa kutembea ...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/11/amfumania-mumewe-asaula.html
HATARI! Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Tatu
Ikoko mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, hivi karibuni alifunga mtaa kwa
kutembea bila nguo baada ya kumfumania mumewe akiwa na mwanamke
mwingine.
Chanzo chetu cha kuaminika kilisema mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake usiku wa Ijumaa iliyopita na aliporejea asubuhi, alimkuta mwenzake akiwa na kigori mwingine ndani ndipo alipopagawa.
“Baada ya hapo tu watu wazima na mashosti zake walimshika na
kumsitiri, akaja bwana’ke akamchukua wakaenda nyumbani kwao,” kilisema
chanzo hicho.
Chanzo chetu cha kuaminika kilisema mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake usiku wa Ijumaa iliyopita na aliporejea asubuhi, alimkuta mwenzake akiwa na kigori mwingine ndani ndipo alipopagawa.
“Alitoka usiku mzima akarudi saa moja
asubuhi akamkuta bwana’ke yuko na mwanamke mwingine ndani, akaanzisha
vurugu, akavua nguo na kubaki na kanga moja na kuanza kupita mtaani huku
akisema nivue nisivue na watu wakawa wanamuitikia vua.
Chanzo kiliendelea kufunguka kuwa tukio
hilo siyo mara ya kwanza kwa mwanamke huyo kwani alishawahi kufanya
hivyo akiwa na mwanamume mwingine aliyejulikana kama Kisiso mtaani hapo
na waliachana kwa tabia hiyo.
“Akiwa na mwanaume halafu akamfumania, ndiyo huwa anafanya hivi na yule
mshikaji wa kwanza kwa aibu ilibidi ahame, sasa hivi anaishi Mbagala,”
kilisema chanzo hicho.imeandikwa na shani ramadhani na mayasa mariwata.

