MSANII DEVOTA ATOA WOSIA NINI KIFANYIKE ATAKAPOKUFA
WAKATI vifo mfululizo vikitokea Mei mwaka huu miongoni mwa wasanii maarufu nchini, nyota wa filamu Bongo, Devotha Mbaga ameibuka na kus...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/06/msanii-devota-atoa-nini-kifanyike.html
WAKATI
vifo mfululizo vikitokea Mei mwaka huu miongoni mwa wasanii maarufu
nchini, nyota wa filamu Bongo, Devotha Mbaga ameibuka na kusema endapo
ataaga dunia, hahitaji kufanyiwa mbwembwe wakati wa msiba na mazishi
yake kama wasanii wengine walivyofanyiwa.
Katika misiba ya hivi karibuni ya wasanii nyota, imeshuhudiwa kamati mbalimbali zikiundwa na kuchangisha fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kununulia majeneza ya bei mbaya, vyakula vya gharama na shughuli zingine ikiwemo ukodishaji wa magari ya kusindikiza msafara wakati wa mazishi.
Msanii maarufu wa filamu Bongo, Devotha
Devotha alisema hatahitaji kununuliwa
jeneza la kifahari, bali lichongwe kwa mbao za kawaida na lisiwekwe
mapambo yoyote, watu wasilie msibani kwake na kwamba endapo vitu hivyo
vitakiukwa, basi mwili wake utagoma kubebeka.
“Unajua duniani nimekuja uchi, sasa siku nikifa sitaki mbwembwe za
kununuliwa jeneza la mamilioni wakati nimeacha watoto, ni bora hizo
fedha wapewe wanangu ziwasaidie, vivyo hivyo pia sitaki watu walie kwa
kuomboleza kwenye msiba wangu kwa sababu watakuwa wananiumiza tu, hata
watoto na ndugu zangu nilishawaambia,” alisema Devotha.Katika misiba ya hivi karibuni ya wasanii nyota, imeshuhudiwa kamati mbalimbali zikiundwa na kuchangisha fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kununulia majeneza ya bei mbaya, vyakula vya gharama na shughuli zingine ikiwemo ukodishaji wa magari ya kusindikiza msafara wakati wa mazishi.
