TMT YASITISHA USAHILI WA VIPAJI KUPISHA MSIBA WA GEORGE TYSON
"TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Proin Promotions Limited ambayo ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents inape...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/tmt-yasitisha-usahili-wa-vipaji-kupisha.html
"TAARIFA KWA UMMA
Kampuni ya Proin Promotions Limited ambayo ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents inapenda kuutangazia Umma wa Watanzania na Wadau wote wa Tasnia ya Maigizo Tanzania kuwa imepokea kwa Masikitiko Makubwa sana taarifa za Msiba wa Mtayarishaji na Muongozaji mahiri wa Vipindi vya Runinga na Filamu, Ndugu George Tyson ambae alifariki Dunia tarehe 30 Mei 2014 kwa ajali ya Gari iliyotokea Eneo la Gairo Mkoani Morogoro akiwa njiani Kurudi Dar Es Salaam.
Ikumbukwe kuwa Kabla ya Taarifa hizo za Msiba kupatikana Shindano la Tanzania Movie Talents lilikua linaendelea katika Kanda ya Pwani ambapo usaili ulianza Tarehe 30 Mei 2014 Saa Mbili Asubuhi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam.
Kutokana na msiba huu ambao pia Umemgusa Moja kwa moja mmoja wa majaji wetu katika Shindano hili Bi Yvonne Cherry au Monalisa ambaye Marehemu alikuwa Mzazi mwenzake na walibahatika Kupata Mtoto mmoja aitwaye Sonia. Tunapenda kuutangazia Umma na Wadau wa Tansia ya Filamu Tanzania kuwa, Sisi Kama wadau wa Filamu Tanzania tumeamua kusitisha Usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents Kwa Kanda ya Pwani mpaka pale msiba utakapomalizika.Lakini vipindi vitaendelea kuruka Kama kawaida..! Tunapenda Kutoa Pole Kwa Familia ya Marehemu George Tyson, Kwa Jaji Wetu Vyonne Cherry na kwa wadau wote wa Tasnia ya Filamu Tanzania. Hakika tumempoteza Mtu mahiri katika tasnia hii ya Filamu na Vipindi vya Televisheni.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi.
AMEN.