TIMU YA TANZANIA MOVIE TALENTS KUWAKILISHWA NA JAJI SINGLE MTAMBALIKE KATIKA MAZISHI YA MAREHEMU ADAM PHILIP KUAMBIANA
Uongozi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited na Timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni Waandaaji na waendeshaji wa...
Uongozi wa Kampuni ya Proin Promotions
Limited na Timu nzima ya Kampuni ya Proin
Promotions Limited ambao ni Waandaaji na
waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie
Talents tunapenda kutoa pole zetu za dhati
kwa Wazazi wa Marehemu Adam P .Kuambia ,
Ndugu wa Marehemu , Jamaa , Marafiki kwa
ujumla na Rais wa Klabu ya Bongo Movie ,
Ndugu Steve Nyerere kwa kuondokewa na
Mmoja kati ya Wasanii Mahiri kabisa katika
tasnia hii ya filamu nchini vilevile tunatoa
Pole zetu kwa Wasanii wa sanaa ya Maigizo
Tanzania na Klabu ya Bongo Movie kwa
kuondokewa na Msanii mwenzao Adam P
Kuambiana.
Kutokana na Msiba huo wa Marehemu Adam
Philip Kuambiana, Uongozi wa Kampuni ya
Proin Promotions Limited ambao ni
waandaaji na waendeshaji wa Mashindano ya
Tanzania Movie Talents unapenda kutangaza
kusitisha Zoezi la Usaili wa Shindano hilo
lililokuwa linaendelea Mkoani Arusha kwa
siku moja kwaajili ya Kuungana na
Watanzania katika Msiba huu Mkubwa
ulioikumba Tasnia ya Filamu Nchini Katika
kuomboleza na Kushiriki katika Mazishi ya
Marehemu Adam Philip Kuambiana
yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumanne
tarehe 20 Mei 2014 katika Makaburi ya
Kinondoni.
Kutoka Kwenye timu ya Tanzania Movie
Talents iliyopo Mkoani Arusha, Timu hiyo
itawakilishwa na Mmoja wa Majaji katika
Shindano la Tanzania Movie Talents , Ndg
Single Mtambalike ambae anatarajia kusafiri
kesho kwa Ndege kutoka Mkoani Arusha
kwaajili ya Kuungana na Watanzania wote na
wasanii wengine katika msiba na mazishi ya
Marehemu Adam Philip Kuambiana . Vilevile
Ndg Single Mtambalike ataungana na
Wafanyakazi wa Proin Promotions Limited
waliopo jijini Dar Es Salaam katika Msiba
huo.
Timu nzima ya Tanzania Movie Talents
iliyopo Mkoani Arusha tunapenda kutoa Pole
zetu za Dhati kwa wafiwa wote na
watanzania wote tulioguswa na msiba huu
wa Msanii wa Filamu Nchini Adam
Kuambiana.
Shindano la Tanzania Movie Talents
litaendelea kama kawaida siku ya Jumatano
asubuhi kama ratiba ilivyopangwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho
ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la
Bwana lihimidiwe
Imetolewa na
Josephat Lukaza
Afisa Mahusiano - Tanzania Movie Talents
Proin Promotions Limited
