TABIA YA LULU KERO BONGOMUVI
WAMEANZA! Tabia ya staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘ Lulu’ ya kutojumuika na wenzake kwenye matukio ya kijamii h...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/tabia-ya-lulu-kero-bongo-muvi.html
WAMEANZA! Tabia ya staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘ Lulu’ ya kutojumuika na wenzake kwenye matukio ya kijamii hasa matatizo inadaiwa kuwakera Klabu ya Bongo Movie Unity hivyo kuandaa kikao maalum cha kumkanya. Staa wa sinema za Kibongo , Elizabeth Michael Kimemeta ‘ Lulu ’.
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini, zilidai kwamba malalamiko hayo ya kuwa Lulu amekuwa mzito kuhudhuria shughuli za wenziye kama misiba au hata sherehe zilianza tangu alipotoka gerezani Segerea,
Dar . Ilisemekana kwamba kilichosababisha viongozi wa Bongo Muvi kukasirishwa na kuamua kumweka kikao ili kumsema, ni kwamba ipo siku naye yatamfika. Baada ya kuzinyaka ‘ niuzi ’ hizo motomoto ,
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwenyekiti wa Bongo Movie , Steven Mengere ‘ Steve Nyerere’ ambaye alikiri kuwepo kwa ishu hiyo ili kumuonya kwa tabia yake hiyo kwa kuwa yeye bado mdogo . Alisema Lulu anatakiwa afuate nyayo za wakubwa zake ambao wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali kwa kuwa ipo siku naye yatamfika. “Lulu ni mtoto mdogo , hatushindi kwa lolote, lazima tumwambie ukweli kuhusu dunia ilivyo na maisha yanavyokwenda . ‘ Lulu ’ katika pozi tofauti . “Sisi kama Bongo Movie tuna kawaida ya kuhudhuria shughuli za wenzetu pale inapobidi lakini kama mtu anakuwa na udhuru huwa anatoa taarifa lakini yeye hana kawaida hiyo , anajiona amekamilika. “Naaamini ipo siku na yeye yatamfika kwa
kuwa mitihani ni kawaida kwa binadamu, sidhani kama mtu atajitokeza na kumuunga mkono kwa tabia hiyo na siyo yeye tu anayejitenga, wapo na wengine wengi lakini yeye bado ni mdogo kwetu huenda hajui
alitendalo ndiyo maana tunataka tumfunze jinsi ya kuishi na watu, ” alisema Steve . Kwa upande wake Lulu alipotafutwa na kuulizwa juu ya jambo hilo hakuonesha mshtuko bali aliwaka : “Huyo aliyesema hivyo atajijua mwenyewe mimi sina shughuli na mtu, aachane na mimi . ”

Uswahili mtupu, kwani kuhudhuria msiba ni uamuzi wa mru na ni jambo la kifamilia kwa sana, wehu tu na waswahili wanabongomovie
ReplyDeletelooh hao bongo movie ni wanafki sana lulu alkuwa na matatizo yakapelekea apelekwe mahabusu hakuna hta mmoja nikiyewai kuskia kaenda kumsaidia au hata kumtembelea zaidi ya dkt cheni na wema kama nakumbuka vzr.hata ningekuwa mie ningeingiwa na nyongo.wakikuona wa nn waone wa kazi gani.labda ndo hcho kilichochangia kuwa mvivu
ReplyDelete