DISQUS SHORTNAME

Solange kuanika ukweli kwenyekitabu Juu ya Ndoa ya Jay Z naBEYONCE

Mdogo wake Beyonce Knowles, Solange ambaye  alimake headlines zaidi mwaka huu baada ya video ya ugomvi wake na Jay Z ndani ya lift kuvuj...


Mdogo wake Beyonce Knowles, Solange ambaye  alimake headlines zaidi mwaka huu baada ya
video ya ugomvi wake na Jay Z ndani ya lift kuvuja amepanga kutoa kitabu kueleza yote
yanayoihusu familia yake na uhusiano kati ya Jay Z na Beyonce.  Kwa mujibu wa Buzz60, kitabu hicho cha Solange kitabeba siri nzito ya familia ya Jay Z na Beyonce ambapo tangu utokee ugomvi wa wazi kati ya wanafamilia hao, kumekuwa na  tetesi kuwa Jay Z na Beyonce wamekuwa na
ugomvi wa mara kwa mara unaochangiwa na tabia ya Jay Z kuendekeza michepuko.
Imeelezwa kuwa kitabu hicho kitaeleza pia ukweli wa uhusiano uliopo kati ya Solange,  Beyonce na baba yao Mathew Knowles ambaye alikuwa meneja wa Beyonce na baadae alimfukuza kazi huku kukiwa na tetesi mbalimbali kuhusu chanzo cha uamuzi wa Beyonce. Hatua hii ya Solange wengi wanaweza
kuichukulia kama sehemu ya kuendeleza kick zaidi ya mwaka huu kwa kuwa baada ya kutoka
video inayoonesha anampiga vibao Jay Z ndani ya lift, ameweza kuteka umakini wa watu wengi
duniani huku ikidaiwa kuwa mauzo ya nyimbo zake.  Hata hivyo, baada ya ugomvi huo, Solange, Jay
Z na Beyonce walitoa tamko rasmi lililoeleza kuwa wameyamaliza kama familia na sasa  wanaendelea na maisha kama kawaida. Mwimbaji huyo wa kike toka Texas ambaye huwa yuko busy kwenye mitandao ya kijamii, amekuwa kimya kwa upande wa Twitter tangu  May 12, siku ambayo video ya ugomvi wake na Jay Z ilivuja kupitia mtandao wa TMZ..

Related

KWINGINEKO DUNIANI 2545299882710212870

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item