DISQUS SHORTNAME

Q Chillah aelezea nini kilitokea kabla ya kifo cha Adam Kuambiana

Msanii wa muziki Aboubakar Katwila aliyekuwa rafiki wa karibu wa marehemu Adam Philip Kuambiana, amedai kuwa kabla ya kifo cha rafiki ya...


Msanii wa muziki Aboubakar Katwila aliyekuwa
rafiki wa karibu wa marehemu Adam Philip
Kuambiana, amedai kuwa kabla ya kifo cha rafiki
yake, alilalamika maumivu ya tumbo ambapo
Ijumaa iliyopita alikuwa akilalamika maumivu ya
tumbo na kuharisha damu.

Profesa Jay,JB ,Q Chillah wakiwa na marehemu
Adam Philip Kuambiana enzi za uhai wake
maeneo ya Coco Beach jijini Dar
Akizungumza na Ijumaa Wikienda alisema: “Jana
(ijumaa) jioni Kuambiana na wasanii wenzake
walikuwa baa wakinywa pombe hadi usiku wa
manane lakini bado akiendelea kulalamika
maumivu ya tumbo. Wenzake walimuuliza ni kwa
nini alikuwa anaendelea kunywa pombe wakati
anaumwa? Akawaambia wamuache. Baada ya
kumaliza kunywa kila mmoja alikwenda kulala
chumbani kwake huku tukiahaidiana kwamba
itapofika saa 3:00 asubuhi tuwe tayari kwa
kwenda location. Lakini ilipofika muda huo sisi
tukiwa tayari kwa safari tulikwenda kugonga
mlango wa chumba chake bila mafanikio.
Chakushangaza alisikika sauti yake kwa mbaili,
kwa bahati nzuri mlango wake ulikuwa wazi,
mmoja akaingia ndani na kumkuta ameanguka
chooni na hajiwezi. Neno lake la mwisho alisema
kwamba anajisikia kuishiwa nguvu na anaharisha
damu. Kutokana na hali yake hiyo mbaya
tulimbeba na kumlaza kitandani kasha tukatafuta
gari na kumkimbiza Hospitali ya Mama Ngoma
ambapo daktari alisema alishafariki dunia muda
mrefu,”alisema Q Chillah
Q Chillah ambaye alikuwa mhusika na filamu
mpya ya ‘Joto’ ya marehemu Adam Kuambiana
amedai kuwa marehemu alisema kuwa filamu
hiyo ambayo waalikuwa wanaifanya ingekuwa ya
mwisho kwake.
“Nimeumia sana kwani hii filamu ndiyo ilikuwa
apate fedha nyingi sana kwa sababu ni yak wake
mwenyewe na ni kali mno, amecheza vizuri
akinishirikisha mimi. Lakini ndiyo hivyo tena
imeishia katikati sijui ni nani ataiendeleza maana
mwenyewe katuachia majonzi,” aliongeza Q
Chillah.
Historia fupi ya Adam Kuambiana
Marehemu Adam Philip Kuambiana alizaliwa
mwaka 1976 Ifunga Mkoani Iringa, alipata elimu
ya msingi katika shule ya Mlimani Jijini Dar na
baade sekondari ya Tambaza kisha akahamia
jijini Nairobi kwenda kusoma kidato cha tano na
sita baada ya hapo alielekea Afrika Kusini kupata
elimu ya filamu na baada hapo alikuwa fiti katika
uwigizaji, uongozaji na pia alikuwa mwandishi wa
miswada ya filamu.
Miongoni mwa filamu ambazo amerehemu ametia
mikono yake kwa kiwango kikubwa ni pamoja na
Fake Pastor, Life of Sandra, Faith ,More Fire,
Scora, Lost Son, My Fience, Jesica, Basilisa, No
Body, Chaguo Langu na nyingine nyingi.

Related

BONGO MOVIE 4642955101490795244

Post a Comment

  1. maua Yassin KatemboMay 19, 2014 at 6:55 PM

    mbele yake nyuma yetu...may his soul rest in peace

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item