Pongezi kwa Jeshi la polisi: Mbwa mwitu 155 ( VIBAKA ) waliolitikisa jiji la Dar kwa uporaji na kujeruhi wakamatwa
Baadhi ya vijana wa kundi la mbwa mwitu waliokamatwa Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dares salaam limefanya msako wa nyumba hadi nyum...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/pongezi-kwa-jeshi-la-polisi-mbwa-mwitu.html
![]() |
| Baadhi ya vijana wa kundi la mbwa mwitu waliokamatwa |
Msako huo uliofanyika ndani ya masaa 24 katika maeneo ya Kigogo, Magomeni, Tabata, Mto msimbazi pamoja na Mbagala. Kupitia msako huo watuhumiwa 149 wamekamatwa ambapo mmoja amegundulika kuwa ni kiongozi wa kundi hilo la Mbwa Mwitu. Kiongozi huyo amefahamika kwa jina la Athuman Said (20) mkazi wa kigogo. Athumani amekiri anaongoza kundi la vijana (mbwa mwitu ) wapatao 15.
![]() |
| Kamanda Kova akionesha picha ya Mbwa Mwitu waliokamatwa |
Imegundulika kuwa vijana hawa waliokamatwa hutumia madawa ya kulevya aina ya Bangi, Sindano pamoja na Mirungi. Vijana hao hupenda kushirki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku, kigodoro, kangamoja na Baikoko. Ngoma hizi huchezwa usiku wa manane, wakitoka ngomani imebainika kwamba hujikusanya pamoja na kutekeleza vitendo vya uhalifu. Baadhi ya majina ya waliokamatwa ni Daniel Peter, Mwinshehe Adam, Mohamed Said, Jakama Alphonce, Hamadi Mdudu, Salumu Musa, Antony Daniel, Fidelin Antony, Hamza Mazuma, Mganga Abeid, Said Abeid, Salum Nyenje, Dominick Peter, Kulwa Abeid, Musa Ibrahim pamoja na Hussein Shaban.



Yan kiongoz ana 20 hao wafuasi?
ReplyDeleteWakatwe mikono yao hao ndo adhabu inayowafaa maanahawataki kujishughulisha wanataka easy going wenzao wanaangaika kutafuta pesa wao wanawarudisha nyuma.
DeleteMbwa mwitu hao waliovaa ngozi ya kondoooo wakatwe mikono yao maana haina faida na wao wapate maumivu kama waliowasababishia wenzao