Mastaa Wa Hollywood Kumkoma Wema Sepetu Kwenye BETAwards 2014, Apanga KuwafunikaKwenye Red Carpet !
Habari mpya ni kuhusu Wema Sepetu kuhudhuria tuzo za BET Awards 2014 ambazo zimepangwa kufanyika hivi karibuni huko Los Angels marekani ...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/mastaa-wa-hollywood-kumkoma-wema-sepetu.html
Habari mpya ni kuhusu Wema Sepetu kuhudhuria
tuzo za BET Awards 2014 ambazo zimepangwa
kufanyika hivi karibuni huko Los Angels marekani
na kuwakutanisha mastaa wa Hollywood
wakiwemo wanamuziki na mastaa wa filamu.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na
Wema ambaye umaarufu wake ni mkubwa
Tanzania kuliko hata baadhi ya viongozi wa
ngazi za juu serikalini kikizungumza na
Swahiliworldplanet leo kimesema kuwa Wema
anajiandaa vilivyo kwenda kufunika mastaa wa
Hollywood katika red carpet ya BET Awards 2014
ambapo mpenzi wake Diamond Platinumz
amependekezwa kuwania tuzo ya Best
International Act, Africa. "nakupa exclusive,
Wema anaji-prepare kwa ajili ya tuzo za BET
Awards 2014, siwajua Nasib(Diamond) anawania
tuzo hizo, basi Wema atatia team
ninavyokuambia ana hakikisha muonekano wake
kwasasa hauna hata kipele cha joto siwajua tena
atakutana uso kwa uso na kina Beyonce na
Rihanna ! basi ataka kuwaonesha kazi kuwa
kuna mademu wakali toka Bongo ha ha ha
haaaa(akiangua kicheko)............chonde chonde
usije ukaniandika jina langu blogini" kilisema
chanzo hicho ambacho pia ni msanii wa filamu
Chanzo hicho kilipoulizwa kuwa je wataenda
Wema na Diamond pekee au na mama Diamond
pia ataenda kumsapoti mwanae kilisema kuwa
mama Diamond anaweza kwenda kuosha nyota
pia lakini Diamond ataondoka na maneja wake
kwa anavyojua kwasasa " hilo sina uhakika kwa
sasa ila nitakujuza usijali but Diamond na Wema
wataenda na management ya Diamond siwajua
ni tukio international, pia Martin Kadinda(meneja
wa Wema) anaweza kwenda"
Alipoulizwa anadhani Wema Sepetu atavaa nini
kwenye red carpet alisema hajui na hayamhusu
hata akivaa gunia shauri yake lakini mbunifu
maarufu nchini Evelylin Rugemalira(Eve
Collections) ana uwezekano mkubwa wa
kumvalisha sababu ndiye anayemuwezea kwenye
red carpet nyingi ikiwemo tuzo za Kilimanjaro
Tanzania Music Awards 2014 Wema alikuwa
kama showstopper "sijui hilo hata akivaa gunia it
is none of my business kikubwa jua ataenda but
kuna yule dada wa Eve Collection nafikiri
unampata basi yule anaweza kumvalisha Wema,
Nakwambia mastaa wa Hollywood
watamkoma......sisi yetu macho tunasubiri picha
mtuwekee" kilisema chanzo hicho chenye
maneno mengi.
Source: swahili world
