Kumbe Solange amefuta picha zake na Beyonce insta akaacha hii tu, tazama alichofanya Beyonce
Kwa wale mnaofatilia stori za mastaa, ikiwa ni chini ya saa 48 toka iripotiwe kwamba Solange ameziondoa kwenye page yake ya instagram p...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/kumbe-solange-amefuta-picha-zake-na.html
Kwa wale mnaofatilia stori za mastaa, ikiwa ni chini ya saa 48 toka iripotiwe kwamba Solange ameziondoa kwenye page yake ya instagram picha alizopiga na dada yake yaani Beyonce, B amejibu kwa kufanya maamuzi ya kuweka kumbukumbu za hizi picha nne alizopiga na Solange.
Mwanzoni ilionekana ugomvi ni kwa Solange na Jay Z ila kuna kitu kinaendelea manake uamuzi wa Solange kufuta picha za Beyonce
kwenye insta yake umekuja baada kusambaa kwa video ikimuonyesha yeye (Solange) akimpiga Jay Z kwenye lift ya hoteli huku Beyonce akiwa pembeni akishuhudia bila kuingilia kati hata kwa kumzuia Solange.
Hii ndio picha pekee Solange aliyokua kaibakiza kwenye instagram yake lakini sasa hivi haionekani na kuna uwezekano ameshaifuta tayari. Saa kadhaa baada ya picha zake kufutwa na Solange, Beyonce alipost picha 4 akiwa na Solange ndani ya saa 17 huku moja tu ndio ikiwa na caption ya ‘good morning’ ila nyingine
hajaandika kitu. Imeripotiwa kwamba hakuna maelewano mazuri kati ya ndugu hawa wawili Beyonce na
mdogo wake Solange. ‘Good morning’ Baada ya Solange kuonekana akimpiga Jay Z kwenye lift zilitoka stori za chinichini kwamba Rihanna ndio chanzo cha yote ambapo Beyonce amezikanusha hizo stori kwa kuweka picha akiwa na Rihanna kuonyesha kwamba kila kitu kiko poa.

