Kim Kardashian Akanusha TetesiKuwa Wameshafunga Ndoa
Siku chache baada ya kusambaa tetesi kuwa Kanye West na Kim Kardashian tayari wamefunga ndoa yao ya kwanza (kiserikali), mrembo huyo ame...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/kim-kardashian-akanusha-tetesi-kuwa.html
Siku chache baada ya kusambaa tetesi kuwa
Kanye West na Kim Kardashian tayari
wamefunga ndoa yao ya kwanza (kiserikali),
mrembo huyo ameamua kusema na kuzikanusha
tetesi hizo.
Bibi harusi mtarajiwa ambaye ataonekana
kwenye TV akiwa na mumewe Kanye West
watakapofunga ndoa rasmi May 24,
ameekanusha tetesi hizo kupitia akaunti yake ya
Twitter.
Tetetesi ya pili aliyoikanusha ni pamoja na ile
inayoaminika sana kuwa ndoa yao itaoneshwa
kwenye show maarufu ya familia yake, “Keeping
Up With The Kardashian”.
Kim K alikanusha pia kuwepo orodha ya wageni
1600 iliyosemekana kuwa na majina mengi ya
watu maarufu akiwemo Lupita Nyong’o, Winnie
Mandela na wengine.
Na mwisho akawatahadharisha watu kuhusu
picha za nguo zake za harusi zinazosambaa
kuwa sio za kweli.
“Seeing fake wedding dress pics of me. No one
has seen my dress! Those photos are old or
photo shopped.”
