DISQUS SHORTNAME

JOHARI AMTUPIA CHUCHUVIJEMBE MSIBANI

STAA wa Bongowood, Blandina Chagula  ‘ Johari’ anadaiwa kumtupia vijembe kiaina  msanii mwenzake , Chuchu Hans ambaye ‘ anabanjuka kimalo...


STAA wa Bongowood, Blandina Chagula  ‘ Johari’ anadaiwa kumtupia vijembe kiaina  msanii mwenzake , Chuchu Hans ambaye ‘ anabanjuka kimalovee ’ na mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya RJ, Vincent Kigosi ‘ Ray The Greatest’ .
Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye msiba wa mwigizaji Sheila Haule ‘ Recho ’ Sinza - Palestina , Dar , hivi karibuni ambapo vijembe viliibuka baada Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘ Nyerere ’ kumuuliza  kwa lugha ya utani Chuchu kuwa RJ itachangia nini msibani hapo, Johari  akadakia:  “Kampuni yangu si ya uchochoroni au ya chumbani , nina TIN namba kabisa siyo kama hiyo nyingine , iweje umuulize asiyehusika.. .”
Baada ya Johari kutamka maneno hayo , waombolezaji waliokuwepo msibani hapo  walipigwa na butwaa na kuhoji kulikoni? Johari amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano  na Ray kipindi cha nyuma huku kukiwa na taarifa kuwa Chuchu ana kampuni iitwayo  Chura ikimaanisha Chuchu na Ray hivyo
ilitafsiriwa kuwa alikuwa akiipiga kijembe kwa madai kuwa haiwezi kufikia levo za RJ.  Alipofuatwa na mwanahabari wetu ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo , Johari hakuwa  tayari kwani alisema ana majonzi ya kuondokewa na kipenzi chake Recho hivyo  hakutaka malumbano na watu katika kipindi
hiki kigumu .

Related

BONGO MOVIE 2888461107614489727

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item