Hits, video kali na muonekanovyote anavyo, lakini hili ni jambo Diamond anatakiwa kulibadilisha
Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wenye neema nyingi kwa Diamond Platnumz kimataifa. Tangu aachie video ya remix ya My Number One aliomshrikish...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/hits-video-kali-na-muonekano-vyote.html
Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wenye neema
nyingi kwa Diamond Platnumz kimataifa. Tangu aachie video ya remix ya My Number One
aliomshrikisha Davido, jina la staa huyo limekuwa
kubwa kiasi cha sasa kumfanya afike sehemu
ambayo hakuna msanii wa Tanzania aliyewahi
kufika.
Diamond akitumbuiza Club Bilicanas Ijumaa iliyopita Kuanzia video yake kushika namba moja kwenye
vitu vikubwa vya TV kikiwemo Trace TV, kutajwa kuwania tuzo za MTV MAMA katika vipengele viwili na pia kutajwa kuwania tuzo za BET kwenye kipengele cha Best International Act:
Africa. “An international music superstar from Tanzania is being born right before our eyes. Hongera sana @diamondplatnumz,” alitweet January Makamba.
Ni kweli, supastaa wa kimataifa kutoka Tanzania amezaliwa mbele ya macho yetu na ni wajibu wetu kumuunga mkono katika kila hatua anayoenda. Lakini kama unamtakia mtu heri na mafanikio zaidi, si lazima kumsifia muda wote. Ni vyema kumwambia ukweli pale ambapo tunahisi
anatakiwa kuparekebisha ili asonge mbele zaidi.Jambo muhimu ambalo Diamond anatakiwa kurekebisha ni katika live performance. Naomba nikiri kuwa pamoja na kuwa shabiki mzuri wa nyimbo nyingi za Diamond, sijawahi kupenda
performance zake za live. Nimeshamhudia kwa
zaidi ya mara 10 akitumbuiza na zote nimekuwa
nikimuona akifanya vilevile na sipati kile ambacho
nakuwa nakitegemea.
Juzi alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza
kwenye show ya Road to MAMA ya MTV Base
iliyofanyika Club Bilicanas akiwa pamoja na Sauti
Sol na kundi la Mi Casa Music. Bahati mbaya
ama nzuri kwake ni kwamba kutokana na kuwa
msanii mwenyeji, yeye alikuwa msanii wa mwisho
kutumbuiza. Walianza Wakenya Sauti Sol ambao
kwa mtu aliyekuwa pale ukumbini atakubali kuwa
show yao ilishangiliwa sana.
Baadaye walifuata Mi Casa Music na wao
wakadhihirisha kwanini ni kundi bora la muziki wa
house kwa sasa nchini Afrika Kusini kwa kupiga
show kali sana.
Diamond alifuata na kama kawaida wakati
anaingia alishangiliwa mno. Kama kawaida yake,
aliungana na dancers wake wanne waliokuwa
wakimpa support. Ilikuwa show ya kawaida
iliyoboa kwa muda mfupi tu.
Ushauri wangu kwa Diamond ni kuwa
asiconcentrate sana katika kucheza na kusahau
kujiimarisha katika uimbaji wa live. Haoneshi
ujuzi wowote wa kuziimba nyimbo zake kiustadi
anapokuwa stejini. Kwakuwa hujikuta akicheza
mno na hivyo kuchoka haraka, sauti yake
huharibika na kusikika vibaya na huondoa kabisa
ule uprofesheno wa sauti ya msanii anayependwa
na mwenye hits nyingi. Kama angekuwa anaimba
na vyombo live show ingekuwa inapewa jeki na
muziki tofauti unaopigwa na bendi.
Atafute namna nyingine ya kiubinifu zaidi ya
uimbaji wa nyimbo zake live. Asitumbuize nyimbo
kama zinavyosikika kwenye CD. Kama ataendelea
na performance za kutumia DJ na CD, basi
atengeneze version tofauti za beats atakazotumia
kuimba live. Madhara ya hiki anachokifanya sasa
ataonekana kama dancer badala ya kuwa
muimbaji, sifa aliyonayo Cabo Snoop.
Kelele na shangwe anazozipata akiwa
anatumbuiza zisimdanganye kuwa anazikonga
nyoyo za mashabiki kwa performance kali
kwakuwa ukweli ni kwamba shangwe nyingi ni
kwasababu nyimbo anazoimba ni hits na wengi
wanazifahamu. Kwa perfomance ya aina ile kama
angekuwa ni msanii asiye na jina, wengi
wasingekuwa wanarespond hivyo.
Shabiki hapendi kwenda kumuona msanii ambaye
nyimbo zake hutumbuiza nyimbo zake vilevile
kama zinavyosikika redioni. Kwa walioshuhudia
show ya P-Square November mwaka jana pale
Leaders Club waliona jinsi mapacha hao walivyo
wachawi wa live performance.
Pamoja na kuwa wachezaji wazuri, hawakuwa
wakicheza katika kila wimbo. Muda mwingi
walikuwa wakiimba nyimbo zao kwa hisia na
kuinteract vizuri na watazamaji.
Kwakuwa kutajwa kwake kwenye tuzo hizo kubwa
kutampa exposure zaidi na kupata show za
kimataifa, alifanyie kazi hilo ili kutowapa sababu
wakosoaji na kumuona kama amebebwa tu kufika
hapo.
Source: Bongo5

Kweli aisee diamond anatakiwa aisome hii kwa umakin na aielewee
ReplyDelete100% i second u mtoa mada ajipange upya kwenye live shows, ikiwezekana awe anaimba na bend hasaa atafute bendi ya kwake uwezo anao kwa sasa
ReplyDeleteNi kweli tupu.. Aisome na akubali kuelewa.
ReplyDeleteSoo true...nakumbuka show yake ya Big Brother...sauti aisee ilikuwa haijajipanga kwa live performance.....
ReplyDeleteKweli kabisa kwanini asiwaachie madansa wake kucheza yy akabakia kuimba na kucheza kidogo
ReplyDeleteuwiii nice speech
ReplyDelete