DISQUS SHORTNAME

DIAMOND AZIDI KUJIWEKA KIMATAIFA ZAIDI, MSOME HAPA

Wiki iliyopita Diamond Platnumz alikua London Uingereza kwa ajili ya kufanya show lakini pia vilevile kufanya video ya wimbo wake aliofany...

Wiki iliyopita Diamond Platnumz alikua London Uingereza kwa ajili ya kufanya show lakini pia vilevile kufanya video ya wimbo wake aliofanya na msanii Iyanya wa Nigeria. AyoTV na millardayo.com zimepata Exclusive interview na meneja Babtale ambae anasimamia kazi za Diamond sasa hivi ambapo amesema kutokana na kupiga hatua kwa Diamond na kuingia kwenye levo za kimataifa, imebidi waanze kufanya video za kiwango hicho cha kimataifa lakini haimaanishi kwamba ndio Platnumz hatofanya tena video Tanzania’ Namkariri Tale akisema ‘video tuliyofanya na Iyanya Uingereza ni kwa sababu tulikua
tunamuhitaji Director MoE Musa ambae anaishi na kufanya kazi zake Uingereza ndio maana tukasafiri mpaka huko, kuna video ambayo tutafanya Nigeria tukishatoka Ghana na pia ikitokea kwamba tunatakiwa kufanya video Tanzania tutafanya hivyo’ AyoTV: Mmetumia kiasi gani cha pesa kufanya hii video Uingereza?
Bab Tale: ‘kiukweli tunaumia, tunaumia kwa sababu kumlipa Moe Musa na kupata kila kitu
kama kwenye hii video ya juzi tumemlipa Moe peke yake dola elfu 25 ambazo zinagonga
mpaka milioni 40 za Kitanzania,
bado usisahau tumewatoa kina Iyanya Nigeria kwa hela yetu kuwaleta London, kuwalipia nauli ya business class kwenye ndege na hoteli hawawezi kulala hoteli mbaya kama sisi watoto wa Manzese’ Kwenye sentensi nyingine, Babtale ameithibitishia millardayo.com na AyoTV kwamba Diamond atasikika tena kwenye kolabo nyingine na Davido itakayowahusisha pia Tiwa Savage wa Nigeria na Mafikizolo wa South Africa ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha TV Afrika.

Related

BONGO FLAVA 2137775142130599756

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item