BINTI ADAI KUBAKWA NA POLICE
DUNIA ina maajabu jamani! Msichana wa miaka 14 ( jina limehifadhiwa) amebakwa huku mwenzake aitwaye Mecy ( 11 ) akipigwa na kuporwa simu na ...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/binti-adai-kubakwa-na-police.html
DUNIA ina maajabu jamani! Msichana wa miaka 14 ( jina limehifadhiwa) amebakwa huku mwenzake aitwaye Mecy ( 11 ) akipigwa na kuporwa simu na mtu aliyedai kuwa ni askari polisi ( kituo hakijulikani ) . Kwa mujibu wa Mecy ( pichani) ambaye ni mkazi wa Kinondoni Msiriri jijini Dar , tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wote walijikuta wakipata dhahama hiyo baada ya kukutana na afande huyo na kuwafanyiavitendo vya kinyama. Msichana wa miaka 14 ( jina limehifadhiwa ) kushoto aliyebakwa huku mwenzake aitwaye Mecy ( 11) akipigwa na kuporwa simu na mtu aliyedai kuwa ni askari polisi ( kituo hakijulikani) .
Akizungumza na Uwazi, Mecy ambaye alipigwa na kuporwa simu alisema : “Ilikuwa saa kumi jioni , mimi nikiwa natembea njiani nilikutana na mwanaume aliyenisimamisha na kusema yeye ni polisi .
Alidai mimi ni mzururaji , baadaye akasema nimemtukana, akaniambia tuongozane kwenda kituo cha polisi . “Tukiwa njiani, alianza kunipiga sana na kunipora simu kisha akanifunga pingu . Mbele tulikutana na rafiki yangu ( anayedaiwa kubakwa mkazi wa Kinondoni- Shamba ) naye akaunganishwa katika msafara ,” alisema Mecy . Mecy aliendelea kusema : “Tuliendelea kuzungushwa na yule polisi kuanzia hiyo saa
kumi jioni hadi giza likaanza “Tulifika sehemu akatupeleka kichochoroni , wakati huo mimi nikiwa bado na pingu . Akaniweka Kwenye kona ya nyumba na kwenda kumbaka mwenzangu.“Baada ya
kumaliza akasema ile ndiyo ilikuwa adhabu ya mwenzangu , mimi adhabu yangu ni kile kipigo na kunipora simu. ” Baada ya simulizi ya Mecy , mwandishi wetu alifanikiwa kuzungumza na anayedai
kubakwa , alikiri kufanyiwa kitendo hicho, akasema: “Nilikutana na ( anamtaja jina) akiwa na huyo
mwanaume ambaye kweli alimpiga na kumpora simu ila sikumuona kama alimfunga pingu, nadhani kwa sababu ya kitete nilichokuwa nacho.” Mwenyekiti wa Mtaa wa Msisiri A , Omar Muhunzi alikiri kupata taarifa hizo za binti hao kufanyiwa kitu mbaya . Alisema baada ya tukio, mabinti hao walikwenda kuripoti Kituo cha Polisi cha Msisiri na kupewa PF 3 yenye namba ya jalada MSR /RB/255 /2014 KUCHUNGUZWA KAMA AMEBAKWA .
Kwa mujibu wa maelezo ya mama yake mdogo wa anayedai kubakwa , binti huyo alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar ambako alilazwa kwa siku mbili na kupimwa akitakiwa kurudi tena baada ya mwezi mmoja . “Kwa sasa tunaelekea Kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kufuatilia ili haki
itendeke , ’’ alisema mama huyo .
