BALOZI WA MALAWINCHINI TANZANIAAFARIKI DUNIA JIJINIDAR ES SALAAM LEO.
Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Flossy Gomile-Chidyaonga (pichani) amefariki dunia leo jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa mud...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/balozi-wa-malawi-nchini-tanzania.html
Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Flossy
Gomile-Chidyaonga (pichani) amefariki dunia leo
jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda
mfupi.
“Ni kwa masikitiko makubwa Wizara ya
Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa (ya Malawi)
unauarifu umma kufariki dunia kwa Balozi
Flossy
Gomile-Chidyaonga baada ya kuugua kwa
muda mfupi jijini Dar es salaam mchana
huu”, imesema taarifa iliyotolewa na msemaji
wa Wizara hiyo Quent Kalichero.
“Tangu mwaka 2006 Marehemu Bi Flossy
Gomile-Chidyaonga alikuwa
Naibu Balozi wa Malawi London kabla ya
kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini
Tanzania mnamo Septemba mwaka 2011”,
imesema taarifa hiyo na kuongezea kuwa
taratibu za mazishi zitatangazwa baada ya
taratibu kukamilika.
