DISQUS SHORTNAME

MDEE NA WENZAKE WAPELEKWA SEGEREA

Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee. Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Cha...

Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee.

Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee na wenzake tisa wamepelekwa katika Gereza la Segerea jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza baadhi ya masharti ya dhamana yao.

Mdee na wenzake nane mapema leo walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kukana tuhuma zinazowakabili.

Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kototii amri za maofisa wa polisi na kufanya maandamano kinyume na sheria Jumamosi iliyopita ya Oktoba 4, mwaka huu.

Watapandishwa tena kizimbani hapo kesho saa 4 asubuhi.

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item