MAJANGA DEREVA NA UTINGO WAJIIBIA MALI WALIZOKUWA WAKISAFIRISHA KWENDA KONGO ZIKIWA NA THAMANI YA TSH MILIONI 100 ,WACHOMA LORI LILILOKUWA NA MZIGO HUO
JESHI la polisi mkoa wa Iringa kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi limefanikiwa kukamata mali za wizi zilizoku...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/06/majanga-dereva-na-utingo-wajiibia-mali.html
Alisema kuwa watu hao waliteketeza lori lenye namba za usajili T527 DPQ likiwa na tela lenye namba T 974 EFE aina ya scania mali ya kampuni ya Dandu ambalo walilikuta likiungua huku silizi zake zikiwa zimefunguliwa na baada ya uchungu wa awali walibaini kuwa lori hilo lilikuwa limebeba mitumba na viatu na baada ya msako ndipo walipofanikiwa kukuta mitumba hiyo ikiwa imefichwa katika nyumba moja kuukuu mali ya mama Gray Mpinga mwenyeji wa Maguhani Mufindi. Alisema kuwa mali hizo ambazo ni mabelo ya mitumba na viatu yalitoka Bandarini kwenda DRC chini ya dereva wa lori hilo ni Enedia Christian (26) mkazi wa Mbeya na utingo wake Deus Gendo (20) mkazi wa Mbeya . Kamanda Mungi alisema kuwa utingo na dereva wa lori hilo baada ya kufika kijiji hicho cha Maguhani walivunja kontena na kushusha mali zote na kuzihifadhi katika nyumba hiyo kabla ya kutafuta mteja na kisha lori kulichoma moto. Alisema kuwa baada ya kufanya wizi huo walitoweka na simu zao kuzimwa na kutokana na jitihada za jeshi la polisi kupitia mtandao wa kimawasiliano wa kuthibiti na wizi wa mitandaoni walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao wakiwa kijiji cha Nyololo. Mbali ya kuwakamata dereva na tingo pia polisi wamekamata watu mbali mbali wahusika wa mtandao huo na kuendelea kumsaka Masko Buhewa mkazi wa Nyololo kwa kuhusika na umilikiwa wa mtandao huo
| Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi kushoto akisalimiana na mwakilishi wa kampuni ya Dandu ambao lori lao limeteketezwa kwa moto |
| Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa akionyesha mitumba iliyohifadhiwa katika nyumba moja Nyololo baada ya kufaulishwa na dereva na utingo wake kisha lori kuchoma moto |
